Wanamuziki wakongwe mazoezini


Kundi la wanamuziki wenye umri zaidi ya miaka 50, wamekuwa katika mazoezi makali tayari kwa kutoa album ya kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wa nchi yetu, na kufanya maonyesho ya muziki. Kundi hili la wanamuziki likiendeleza wazo lililoanza mwaka jana  baada ya wanamuziki kadhaa kufanya onyesho moja katika ukumbi wa Karimjee. Onyesho hilo ambalo lilikimbiwa na wafadhili katika dakika ya mwisho liliendelea kufanyika kwa mafanikio na kuongeza nia ya wanamuziki kufanya maonyesho kama hayo kila mwaka. Baadhi ya wanamuziki ambao wamekuwa katika mazoezi hayo ni Waziri Ally’ Kissinger’, Juma Ubao’King Makusa’, Kikumbi Wanzampango ‘King Kiki’, Hamza Kalala ‘Komando’, Mafumu Bilali Bombenga’Super Sax’, Kanku Kelly’King of Stage’, Akuliake Salehe’ King Maluu’, Juma Omari’Disco’, Kasongo Mpinda Clayton, Kabeya Badu, John Kitime, Andy Swebe’Ambassador, Mohamed Mrisho ‘Moddy’, Juma Sangula, Matei Joseph, Abdul Alvador 'Father Kidevu' na wengineo wengi.
Pamoja na kutunga nyimbo mpya pia kumekuweko na  mazoezi ya nyimbo ambazo wanamuziki hao walizipiga wakiwa katika bendi mbalimbali hapa nchini, mazoezi haya yamekuwa yanatembelewa na watangazaji wa vyombo mbalimbali na wasanii wa kutoka fani mbalimbali, kweli hapa ni mkusanyiko wa wakongwe.


Abou Mwinchumu

Akuliake Salehe 'King Maluu'

Kasongo Mpinda na King Kiki

Maluu katika pozi, wanaita swaga siku hizi


Kabeya Badu na Kasongo Mpinda


Hamza Kalala 'Komando'

Andy Swebe'Ambassador'

Comments