The BEE GEES |
Robin Hugh Gibb, mwanamuziki wa kundi maarufu la BEE GEES amefariki. Robin alizaliwa tarehe 22 Desemba mwaka 1949. Kundi la Bee Gees lilianzishwa kwa
pamoja na pacha wake Maurice na kaka yao Barry japo Robin ndie aliyejulikana
zaidi katika kundi hili. Wazazi wao walikuwa Waingereza japo kwa kipindi fulani
walihamia Australia. Inasemekana kundi hili ndilo lililokuwa na mafanikio
kuliko kundi lolote jingine la Pop duniani. Kwa karibu miongo 6 kundi hili
limekuwa jukwaani. Kundi liliweza kuuza zaidi ya santuri milioni 200.
Watanzania wengi walianza kuwafahamu baada ya kusikia vibao
vyao kama Staying Alive, Night Fever, How deep is your love na kadhalika katika filamu ya filamu ya Saturday
Night Fever.
Tarehe 20 May 2012 Robin
amefariki baada ya matatizo ya muda mrefu ya kansa ya utumbo. Pacha wake
Maurice alifariki kwa tatizo hilohilo 2003.
Grammy Awards za BeeGees
1977
Best Performance by a Group — "How Deep Is Your Love"
1978 Best Performance by a Group — "Night Fever"
1978 Album of the Year — "Saturday Night Fever"
1978 Producer of the Year — "Saturday Night Fever"
1978 Best Arrangement of Voices — "Stayin' Alive"
2000 Lifetime Achievement Award
2003 Legend Award
1978 Album of the Year — "Saturday Night Fever"
1978 Producer of the Year — "Saturday Night Fever"
1978 Best Arrangement of Voices — "Stayin' Alive"
2000 Lifetime Achievement Award
2003 Legend Award
Comments