Tamasha kubwa la Karibu International Music Festival,
litafanyika katika viwanja vya TASUBA Bagamoyo kuanzia Novemba 7-9 Mwaka huu wa
2014.
Vikundi zaidi ya 30 na wasanii zaidi ya 500 kutoka kila kona
ya dunia wanataraji kushiriki.
“Lengo kuu la Tamasha, pamoja kukazia katika kurasimisha
tasnia ya muziki kuwa na umakini zaidi, lakini kingine ni kukuza uchumi wa eneo
husika la Bagamoyo ambalo ni la kihistoria, pamoja na kuhakikisha sanaa ya
asili ya mtanzania inapata kuonekana katika jukwaa la kimataifa,”alisema Lupia.
Katika tamasha hili kila kitu kitakuwa ‘live’ hakutakuwa na
playback Pia kutakuweko na warsha mbalimbali kwa ajili ya wanamuziki na wadau
watakao hudhuria.
Comments