Msanii maarufu nchini Tanzania, Muarabu wa Dubai (a k a Mpoki), ametua
katika Jiji la Frankfurt na kuelekea moja kwa moja katika jiji la maraha
Aschaffenburg ambapo atalala usiku mmoja na kuendelea na safari siku ya
pili kuelekea Berlin ambapo atahudhuria mkutano mkuu wa
Umoja wa watanzania Ujerumani (U T U), Kongamano la biashara pamoja na
sherehe za Muungano wa Tanzania.
Mpoki alitua katika uwanja wa kimataifa wa Frankfurt mnamo saa 10:30
alasiri na ndege ya shirika la ndege la Ethiopia Airlines akitokea Dar
es salaam kupitia Addis Ababa. Msanii huyo alipokelewa na mwenyekiti wa Watanzania nchini Ujerumani.
Comments