PFJ International Band Band ya wanamuziki ndugu



Katika pita pita  mitaani nimekutana na bendi mpya yenye mambo mapyaaa. 
Maeneo ya Sinza Mori karibu na petrol station ya Big Bon katika bar inaitwa Advantage Center nimekuta bendi ikifanya mazoezi makali, lakini bendi hii inatofauti na bendi nyingine, ni bendi ambayo idadi kubwa ya wanamuziki ni ndugu. Jina la band hii mpya ni PFJ International Band….PJF ni kifupi cha Peter Fred na Joseph. 






Joseph Kanuti- Anapiga solo, rhythm na bezi gitaa kasha pitia bendi nyingi sana kati ya hizo ni Mingomase Band iliyokuwa inaongozwa na mwanamuziki Kabatele, Tacosode Bnad, Bantu Group MCA International, DDC Mlimani Park Orchestra(Sikinde), Double M Sound, African Stars Band(Twanga Pepeta),African Minofu Band(Sumu ya Mamba),Almasi Band.


Peter Kanuti

Samson mwimbaji
Peter Kanuti-anapiga rythm na solo gitaa, amepitia bendi zifuatazo, Bantu Group,Vijana Jazz, bendi ya Saida Karoli, Manchester Band


Kasuku mwimbaji kapitia Tango Stars , Afriswezi Band


Adam Lyelu mwimbaji kaimbia Mingomase Band, Kulingalinga Band ya Tandika.



Freddy Kanuti-Anapiga Bass Guitar, Afro Swezi Band ya Marehemu Mzee Mponda, TZ Brothers Band


Paul Kanuti-Drummer, African Minofu Band, Motomoto One Band ya Arusha, Manyara Muzika ya Katesh.





Sembuli Kanuti-  Mpiga drums,kapigia  Highclass Muzika ya Tunduma, African Minofu Band


Comments