MISIBA YA WASANII YAIANDAMA NIGERIA

RIP Enebeli Elebuwa

Justus Esiri
Msimu wa misiba unayoikumba tasnia ya burudani nchini Nigeria unaendelea. Baada ya msiba wa Mzee Enebeli Elebuwa, aliyefariki katika hospitali huko India tarehe 5 Desemba 2012 na kuzikwa January 11 2013, kukafuatia kifo cha mwanamuziki Goldie wiki chache zilizopita, wiki iliyopita Jumatano 20 February Mzee Justus Esiri amefariki katika hospitali baada ya kupata matatizo yaliyotokana na kuwa na kisukari. Esiri alikuwa na miaka 71, alizaliwa November 20, 1942.Umaarufu wa Esiri ulianza miaka ya 70 kutokana na tamthiliya maarufu vya Nigerian Televion Authority iliyoitwa The Village Headmaster, ambapo yeye alikuwa ndie mwalimu mkuu katika tamthiliya hiyo. Marehemu Esiri akiwa na mkewe Omiete walizaa watoto sita, mmoja wao aliyekuwa daktari wa meno aliacha fani hiyo na kuingia katika muziki na anajulikana kama Dr SID.
Mungu Amlaze pema Amen

Comments