Leo tarehe 25 Februari mwaka 2013 ndio ilikuwa iwe siku nyingine ya
kihistoria katika medani ya muziki wa kizazi kipya.
Kwa siku kadhaa sasa tumekuwa tukitangaza kwamba wimbo mpya wa MwanaFA ulio katika
mahadhi ya Hip Hop uitwao “Kama Zamani” aliowashirikisha Man'dojo,
Domokaya na The Kilimanjaro Band (Wana Njenje) ungeanza kuuzwa kupitia
njia mbalimbali kama ‘iTunes’, ‘Amazon’ na kupitia katika simu za
mkononi.
Pia ndio tarehe ambayo Kama Zamani ingeanza kusikika katika vituo vya redio Tanzania na nchi za jirani.
Lifeline Music Inc. ndiyo inayosimamia muziki wa MwanaFA kwa sasa, ikiwa
ni kampuni ambayo inafanya kazi za muziki, kuangalia na kuhakikisha
kwamba wasanii inaowasimamia wananufaika kwa kiasi kikubwa kutokana na
kazi zao; na kwamba muziki unaofanyika kwa sasa unafuata kanuni zote
zinazosimamia makubaliano ya biashara.
Kama mjuavyo, biashara yoyote ina pande mbili na mafanikio yake
yanategemea zaidi maridhiano baina ya pande hizo na utimizaji wa
vipengele tofauti ndani ya mikataba ya biashara.
Katika kuboresha maslahi ya wanamuziki husika na wimbo huu,pia kuboresha
zaidi njia zitakazotumika kuhakikisha ya kwamba burudani hii itawafikia
washabiki wengi zaidi wa muziki unaofanywa na MwanaFA, Kilimanjaro
Band(Wana Njenje) na Man’Dojo na Domokaya, tumefikia uamuzi wa kusubiri
na kusogeza mbele siku ya kuachia wimbo wa Kama Zamani kama
ilivyopangwa hapo awali.
Tunachukua nafasi hii kuwaomba radhi mashabiki ambao mmekuwa mnasubiri
kwa hamu kusikia ni nini muungano huu wa muziki wa kizazi kipya na moja
ya bendi kongwe kabisa za muziki yenye miaka zaidi ya 40 katika tasnia
ya muziki Tanzania umewaandalia.
Kwa niaba ya MwanaFA, uongozi wa Lifeline Music Inc. unaomba uvumilivu
na subira toka kwenu mashabiki na wapenzi wa muziki. Tunaamini kwamba
subira huvuta heri na mambo mazuri hayahitaji haraka.
Tunawashukuru kwa dhati kwa ushirikiano wenu.
Henry Mdimu
PR Strategist
Lifeline Music Inc
-
-
Henry Mdimu Mgaya
Blogger
www.mdimuz.blogspot.com
Entertaniment Editor
Mwananchi Communications
Limited
P.O BOX 19754,
Dar es Salaam
Cell:
+255 787 000 880
+255 767 000 880
+255 715 000 881
Comments