TANZANIA LIVE MUSIC FESTIVAL BEGINS WITH HIGH HOPES

Mbegu mpya imepandwa leo katika anga za muziki ‘live’ Tanzania. Kwa mara ya kwanza kabisa Tamasha la muziki lililoprwa jina la Tanzania Live Music Festival limeingia anagani na kuonyesha kuwa Tanzania ina weza na ina nafasi ya aina hii ya Tamasha. Tamasha hili lililotayarishwa na Edge Entertainment ambalo litadumu kwa siku mbili na kupandisha jukwaani zaidi ya bendi kumi na mbili, lilitegemea kupata gedha ambazo zingesaidia kutunisha mfuko wa CHAMUDATA ili kiweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na pia kuupa nafasi inaostahili muziki wa dansi Tanzania.. Kama alivyosema taxi driver wa taxi iliyonirudisha nyumbani kuwa kwa mwendo huu muziki wa dansi utarudi hewani. Waliopanda jukwaani kwanza walikuwa ni Msondo Ngoma Music Band, ambao walifungua dimba kwa kupiga vibao kadhaa ambavyo kati yao viliimbwa na mkongwe mzee Gurumo. Kisha wakapanda vijana machachari wa Mashujaa Musica, waliofuatiliwa na FM Academia , ilikuwa raha tupu. Waliofuata kupanda jukwaani walikuwa ni kundi zima la Mashauzi Classic ambapo wimbo wa kwanza uliimwba na mama mzazi wa Isha Mashauzi mwenyewe, ambaye hatimae alimpa nafasi binti yake katika wimbo wa pili, Raha iliendelea mpaka usiku wa manane kwa bendi za Orynx na K Mondo Sound kuendelea kuburudisha. Baadhi ya bendi ambazo zitapanda jukwaani Jumamosi ni pamoja na Mlimani Park,Wazee Sugu, Khadija Kopa na kundi lake, B Band na pia bendi mpya ya Skylight Band
PANGAMAWE- MSONDO

MASHUJAA

MASHUJAA

MASHUJAA

WAPENZI WA MUZIKI

WAPENZI WA MUZIKI

WAPENZI

MASHAUZI CLASSIC


MSONDO

MSONDO

MSONDO

MSONDOMASHUJAA

KALNAL TOP

MASHUJAA

WAPENZI WA MUZIKI

SOUND ENGINEERS

QUEEN SUZY

FM ACADEMIA DANCERS


FM ACADEMIA

FM ACADEMIA

FM ACADEMIA

FM ACADEMIA

NYOSHI


JACQUELINE WOLPER(BALOZI WA TAMASHA) NA BEN KINYAIA (MC WA TAMASHA)

MPENZI WA MUZIKI

BEN KINYAIYA

MASHAUZI CLASSIC

MAMA YAKE ISHA MASHAUZI


ISHA MASHAUZI

MASHAUZI CLASSIC

MASHAUZI CLASSIC

MASHAUZI CLASSIC

Comments