Simon Mwakifwamba Rais
wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) na
John Kitime Mwenyekiti wa Tanzania Musicians Network)(TMN)
siku ya Jumatano walikuwa na kikao kirefu na viongozi wa juu wa Tanzania
Dancers Association (TDA). Mkutano huo uliokuwa umepangwa na viongozi wa TDA
ulikuwa na madhumuni ya kupata experience ya uongozi wa vyama kutoka kwa
viongozi hawa ambao wamekuwa wakiongoza vyama kwa muda mrefu. Pamoja na mengine
yaliyoongelewa lilikuweko swala kubwa la kuhakiki kuwa TDA wairudie Katiba yao
na kuifanyia marekibisho makubwa. Jambo ambalo viongozi wa TDA waliona walipangie
ratiba na kupata msaada kutooka
kwa viongozi hao wawili.
TDA ni chama kipya cha madansa ambacho kinashirikisha kila
aina ya madansa, tayari kuna matawi ya Mkoa na wilaya tatu za Dar es salaam.
Comments