Kilimanjaro Band (Wana Njenje),Ab kila Jumamosi huwa Salender Bridge

Abou Mwinchum-Percussions and vocals hapa akiimba kibao cha Kiaarabu Habiby

Mohamed 'Moddy' Mrisho- Guitar na vocals

Keppy Kiombile, Bass Guitar, Vocals, na sound engineer anaetegemewa na wengi Tanzania

John  'JFK' Kitime- Guitar na vocals

Waziri Ally Keyboards na Vocals
Kila Jumamosi kuanzia muda wa saa nne mpaka saa kumi usiku Kilimanjaro Band huporomosha muziki pale Salender Bridge. Kuna jambao la kufurahisha katika maonyesho haya, bendi hii ilianza 1974, hivyo kwa sasa ina umri wa miaka 38. Jambo ninalosema la kufurahisha ni kuwa asilimia kubwa ya wapenzi wa Njenje hawajafikia hata umri wa bendi hiyo. Vijana wenye nusu au chini ya nusu ya umri wa bendi ndio wapenzi wakubwa ambao hukesha kila Jumamosi na bendi hii.

Comments