Katika shughuli za sanaa ile ambayo ni ya mapokeo kwa mfano muziki , filamu na kadhalika, wasanii hujikuta wanaiga mambo mengi kutoka kwa wale ambao wanawachukulia kama ni mfano wa mafanikio. Wasanii wa hapa nchini hawapo tofauti na wasanii wenzao wa sehemu nyingine kwani nao pia huiga mengi kutoka kwa wasanii wanaoona hasa kutoka nchi za Magharibi. Uvaaji, ulaji unywaji, na maisha kwa ujumla. Lakini katika kuiga huko kuna mengi yanaigwa ambayo wasanii ingekuwa vyema kama wangefahamu maana yake kwani si nzuri hata kidogo.
Katika historia ya wasanii kumekuwepo na hadithi nyingi za wasanii kuuza roho zao kwa shetani , au kuabudu shetani (Devil Worship), ili waweze kupata mafanikio kisanii. Uanachama wa Illuminati, Devil Worship, Satanism(Kanisa la shetani), 666 na kadhalika, umekuwa unatajwa kuhusiana na watu maarufu wengi kati nchi za magharibi. Ili kuonyesha uhusiano wao na vikundi hivi wasanii hawa huonyesha alama nyingi kwa kutumia miili yao au hata katika picha za album zao au maneno ya nyimbo zao, au vipande vya video zao. Bahati mbaya wasanii wa hapa kwetu wamekuwa wanatumia alama hizo kuonyesha kuwa nao ni wakisasa bila kujua maana za alama hizo. Vikundi hivi ambavyo vinatokana na imani ya kumpinga Mungu hufanya yote machafu ambayo yanakatazwa na Mungu. Hivyo kuiga kila kitu kwa wasanii wetu kama vile utumiaji wa madawa ya kulevya , kutembea uchi ni vitendo haswa vinavyoonyesha uanachama wa makundi haya. Hebu angalia baadhi ya alama zitumikazo kusifia uovu. WASANII CHUNGENI MNAYOYAIGA
Comments