BASATA YATOA ZAWADI KWA WALIOFANYA VIZURI MASOMO YA SANAA KATIKA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE



Kwa  mara ya kwanza Baraza la Sanaa la Taifa limetoa tuzo mbalimbali kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihano wa Taifa wa kidato cha nne. Utaratibu huu uliwahi kuweko miaka mingi iliyopita lakini tuzo zilienda tu kwa waliohitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam miaka mingi iliyopita.
Wanafunzi bora katika mitihani ya sanaa kutoka shule za sekondari za Makongo, Loyola, Azania zote za Dar es Salaam, Arusha Secondary, Bukoba Secondary na Darajani Secondary ya Kilimanjaro, walipata veti na kila mmoja kuondoka na kitita cha shilingi 250,000/- na pia Shirikisho la Sanaa za Ufundi liliongeza a vifaa vya kuchorea kwa washindi hao. Washindi hawa ndio waliokuwa wanafunzi bora katika mitihani yao Kitaifa.
Shule ambazo wanafunzi hawa walitoka pia zilipata vyeti na waalimu wa masomo pia walipata tuzo. Washiriki walisimama kwa dakika moja kumkumbuka mwalimu wa sanaa Sister Elizabeth Justin ambaye alikuwa mwalimu wa muziki wa shule ya Loyola na ambaye kwa miaka miwili mfululizo alitoa wanafunzi bora Kitaifa, na ambaye alifariki mwaka jana. Wanafunzi hawa walifanya vizuri katika masomo ya muziki, fine art, sanaa za maonyesho na msichan pekee ambaye alitokea shule ya Darajani huko Kilimanjaro alifanya vizuri kwenye Sanaa za Maonyesho.
Ombi kubwa la wadau lilikuwa ni masomo ya Sanaa kujumlishwa kwenye kutoa madaraja kama ilivyo kwa masomo mengine.

Comments