Mwanamuziki
muimbaji mahiri Judith Wambura (kulia) maarufu kwa
jina la Lady Jay Dee ametambulisha rasmi kipindi chake kipya cha luninga kitakachoitwa ‘Diary ya Lady
Jay Dee’.
Mkuu wa Vipindi wa East Africa TV Bi. Lydia Igarabuza(kushoto), akiwa na Lady Jay Dee |
Jay Dee amesema madhumuni ya
kipindi hicho ni kuleta burudani tofauti kwa wapenzi wa muziki wake, na muziki
wa kizazi kipya kwa ujumla, vilevile kitatoa fundisho na changamoto kwa wasanii
chipukizi kujua wasanii wakongwe wamepitia katika vikwazo gani.
Kipindi hicho kitakuwa hewani East africa Tv-Channel 5, Jumapili
saa 3 usiku kuanzia Novemba 18.2012
Comments