WASANII WAIJIA JUU COSOTA NA BODI YA FILAMU

SHESHE la aina yake limeibuka baada ya wasanii wa filamu nchini kutoa tamko kuwataka viongozi wa Chama cha Hakimiliki (COSOTA) na Bodi ya filamu kuachia ngazi kutokana na kushindwa kushughulikia matatizo yao......Hayo ndio maelezo kutoka katika gazeti moja la kila wiki kuhusu mvutano kati ya wasanii wa filamu na viongozi hawa wawili. Katika vipindi viwili vya TV vilivyorushwa TBC na kingine EATV, ambacho kilikuwa 'live', wasanii chini ya Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji nchini Mike Sangu, waliueleza ulimwengu juu ya adha wanazozipata kutokana na vipengele vilivyomo katika Kanuni za Bodi ya filamu, na pia kueleza jinsi wasivyo na imani na Justus Mkinga, Mtendaji Mkuu wa COSOTA. Kwa maelezo a picha zaidi ingia HAPA

Comments