John Kitime Katibu Mkuu Shirikisho la Muziki Tanzania |
Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania leo amemtangaza John
Kitime kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo. Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho hilo
ulifanyika mwezi wa pili na vyam 8 vya Shirikisho hilo kuchagua viongozi wake.
Nafasi ya Katibu Mkuu ilikuwa wazi. John Kitime ni mwanamuziki wa bendi ya
Kilimanjaro (Wananjenje), ambaye miaka ya 90 alikuwa Mwenyekiti wa CHAMUDATA na
wakati huo chama kilikuwa katika ufanisi mkubwa wa kuweza hata kuwa na
ushirikiano na mashirika ya miasaada ya nje yaliyowezesha chama hicho kupata
misaada mbalimbali, na hata kufanya matamasha makubwa ya muziki. Pia Kitime ni
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki chama ambacho pia kimewezesha wanacham wake
kupata bima ya Afya. Kwenye mkutano na waandishi wa habari, Katibu Mkuu huyo
alisema kati ya mambo atakayoanza
nayo ni kuimarisha Shirikisho kwa kuimarisha vyama wanachama wa Shirikisho,
ikiwemo kuhamasisha kuanzishwa vyama vingine. Kuonyesha kuwa anania ya
kutekeleza hizo mwisho wa mkutano huo aliwahamasisha waandishi wa habari za
muziki kuanzisha chama chao. Vyama vilivyo wanachama wa Shirikisho la Muziki
Tanzania ni Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania CHAMUDATA, Chama cha Muziki wa
Rumba CHAMURUMBA, Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania CHAMUITA, Tanzania Folk
Music Development Association TAFOMUDEA, Tanzania taarab Association TTA,
Tanzania Urban Music Association TUMA
Comments