FFU wa Ngoma Africa Band jukwaani tena


Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani Ulaya "Ngoma Africa Band" aka FFU
yenye masikani yake nchini Ujerumani, inatazamiwa kutumbuiza katika maonesho ya
Afrika & Orient  Festival, katika Burg Satzvey jirani na miji ya Bonn na Koln,nchini
Ujerumani. Onyesho hilo litakuwa siku ya Jumamosi 28 Mei 201, kuanzia saa 1.00 usiku.
Kamanda wa kikosi kazi hiko Ras Makunja wa FFU atakiongoza
kuhakikisha kuwa gwaride la muziki linamfikia kila mshabiki. Bendi hiyo ina  wanamuziki wenye vipaji wakiwemo wacharaza magitaa wakali kama
vile Chris-B, Said Jazbo Vuai, Maxime Buanda, na wengineo.

Wasikilize zaidi ukiingia
 www.reverbnation.com/ngomaafricaband
au www.myspace.com/thengomaafrica

jiunge nao www.ngoma-africa.com

wasiliana nao kupitia contact@ngoma-africa.com

Comments