HADHARANI MSANII MAARUFU ANATEGEMEA USHIRIKINA

Ushikina ni moja ya mila za kawaida sana kwetu Tanzania. lakini mara nyingi huwa kuna dhana kuwa jambo hili washiriki wake ni watu wazima wa zamani na vijana wa kileo hawashiriki kabisa mambo haya.
Lakini taarifa zilizoifikia blog hii zinaonyesha kuwa jambo hili bado ni muhimu katika maisha ya vijana ambao kwa kila taswira wana maisha ambayo ni mfano kwa vijana wengine na wana majina yanayoheshimika katika jamii.
Taarifa zimefika za msanii maarufu kukesha usiku akifanya shughuli za uganga kwa mganga mmoja Mburahati, mganga huyo ambaye taarifa zinasema kuwa awali alizawadiwa pikipiki kwa kazi hiyo na karibuni kapewa gari aina ya Opa kama malipo kwa shughuli zake hizo. msanii huyo kabla alikuwa akifika hapo hata mchana lakini kutokana na kufahamika na kuona anasindikizwa na watoto wa mtaa mzima wakati akielekea kwa mganga akalazimu kubadili ratiba na kuanza kufika maeneo hayo baada ya giza kuingia
Habari za ziada ni kuwa wasanii wengi wenye heshima katika jamii huonekana kwa mganga huyo kijana. Ambaye hapo Mburahati kaweka ofisi tu ya kazi mwenyewe haishi hapo.
Ushauri kwa wasanii, mazoezi, mipango bora na kufuata masharti ya kazi hii ya sanaa, na kikubwa kuliko yote kumuweka Mungu kuwa kiongozi wa shughuli zako ndiko kutakako kuhakikishia kudumu kwa muda mrefu katika tasnia hii. Ingekuwa ushirikina ndio jibu, ni wazi tungekuwa na nyimbo kwenye Top Ten za dunia.

Comments