Mnyupe & Roma |
Msondo ngoma Group 'Baba ya muziki' imepanga kufanya ziara ndefu katika mikoa mbalimbali kuanzia April 21 mwaka huu. Ziara hiyo itaanzia katika mji wa Morogoro ambapo bendi itatumbuiza Savoy Inn tarehe April 21 usiku na tarehe April 22 bendi itakua Iringa katika ukumbi wa New Life Night Club na tarehe 23 April bendi itakuwa Makambako katika ukumbi wa Midtown.
Bendi itaelekea Songea mkoani Ruvuma ambako tarehe 24 April kutafanyika onesho kubwa katika ukumbi wa Serengeti Bar. Tarehe 25 pia kutakuwa na onyesho jingine hapohapo Songea. Tarehe 26 bendi itakuwa Tunduru, na tarehe 27 moto utawaka Masasi katika ukumbi wa MADEKO
Msondo watakuwa Newala April 29 katika ukumbi wa Blantaya, wakati kesho yake April 30 Msondo wataweka mambo hadharani katika ukumbi wa Oceanic wa mjini Lindi na kuanza kurejea Jijini Dar es Salaam.
Msondo watakuwa Newala April 29 katika ukumbi wa Blantaya, wakati kesho yake April 30 Msondo wataweka mambo hadharani katika ukumbi wa Oceanic wa mjini Lindi na kuanza kurejea Jijini Dar es Salaam.
Roma &Nzawisa |
Comments