Samwel Mshana maarufu kama Mshana Bass, aliyekuwa mpiga gitaa la bezi katika kundi la TOT amefariki dunia leo alfajiri. Samwel
alikuwa amelazwa hospitali baada ya ajali, ambapo pikipiki aliyokuwa akiendesha
iligongana na bajaji maeneo ya Mwananyamala Komakoma. Kifo chake kimekuwa cha
ghafla na kushangaza kwa kuwa kwanza ajali haikutokea kwenye mwendo kasi na
baada ya ajali hakuonekana kuwa na majeraha yoyote makubwa, na hata siku ambazo
rafiki zake walikuwa wakimtembelea hospitali hakuonyesha dalili kuwa ni jambo
kubwa. Kazi ya Mungu haina makosa.
Mungu amlaze pema SAMWEL MSHANA
Comments