Isha Mashauzi ni mwanamuziki wa Taarab ambaye atakumbukwa na wana historia wa muziki kwa mambo ambayo inawezekana hata yeye hajajua ukubwa wake. Kwanza Isha anatokea Mkoa wa Mara, mkoa huu hauonekani kabisa kama unaweza kuwa na uhusiano na muziki wa Taarabu, Isha amekwisha tunga mpaka wimbo wa kusisitiza hilo wimbo huo unajulikana kama Isha Mtoto wa Musoma. Mavazi ya Isha yamekuwa yakileta mazungumzo katika jamii ya wapenzi wa Taarabu, na sasa ameenda mbale zaidi, katika Taarab hii ambayo wahusika huiita modern Taarab, na wapinzani wake wanasema hii sitaarabu kabisa, pamoja na kuweko na vijana wacheza show katika kundi lake, kwa mara ya kwanza tunamuona mwimbaji wa muziki huu nae akijiunga na wacheza show na kucheza nao step zao. Isha kafungua ukarasa mpya katika muziki huu
Comments