Simon na sequencer Kalabash Bar Mwenge


Simon
Rafiki yangu mmoja alinipigia simu na kunambia njoo hapa Calabash Mwenge ufaidi, kuna bendi inapiga nyimbo za bendi ya Tancut. Nilipowasili toka nje nikasikia kibao cha zamani cha DDC Mlimani park, nikajiuliza nani hawa. Nilipoingia nikamkuta rafiki yangu Simon na mwenzie. Simon akiwa kwenye keyboards na mwenzie guitar, na wote wakiimba huku vyombo vikipiga kwa mtindo wa sequencer. Walikuwa wanapiga vizuri sana. Nikakumbuka mbali sana. Nikamkumbuka Simon alipokuwa mdogo, mwanzoni mwa miaka ya 90, akawa anakuja Vijana Jazz enzi za Vijana Day na kuingia katika mashindano ya kuimba tuliyokuwa tunayawafanya wakati huo. Watoto kwa wakubwa walikuwa wakishindana kuimba nyimbo za Vijana na mshindi kupewa zawadi mbalimbali, kama radio, ndoo, kanga sahani saa za ukutani na kadhalika. Simon alikuwa akishinda mara kwa mara, kwa sasa ni mwanamuziki wa hali ya juu ambae amekwishafanya ziara nyingi nchi za nje. Juma Katundu wa Msondo nae ni zao la mashindano hayo

Comments