Tanzania Moto Modern Taarab kuzinduliwa Oktoba 28

 Bendi Kongwe nchini, Msondo Ngoma na bendi inayokuja juu katika wigo wa muziki wa dansi Mapacha Watatu watakuwa pamoja na kundi jipya la Taarab la Tanzania Modern Taarabb (T-Moto) ‘Real Madrid’ katika uzinduzi wa kundi hilo utakaofanyika Oktoba 28,2011 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Mkurugenzi wa kundi hilo la Tanzania Modern Taarab, Amini Salmini, alisema kuwa  uzinduzi wa kundi hilo utafanyika sambamba na uzinduzi wa albam yao kwanza ya inayokwenda kwa jina la Aliyeniumba Hajanikosea.

Comments