Friday, March 16, 2012

Benny Omar na Abou Omary wafiwa na baba yao

Ben Omary

Abuu Omary
Wanamuziki waliopo juu kama ilivyokuwa imeelezwa awali katika blog hii wamefiwa na baba yao mzazi Mzee Omar Abubakar Njenga,baada ya kuugua tangu mwishoni mwa mwaka jana(2011). Kifo kimetokea katika hospitali ya Lugalo na mipango ya kuusafirisha mwili kwenda Nachingwea kwa mazishi inafanywa nyumbani kwake Mbagala.
Mzee Njenga alikuwa mfanya kazi wa Agip (T)Ltd(enzi hizo), hadi alipostaafu 1992,alikuwa kikazi zaidi makao makuu mtaa wa Msimbazi/Mkunguni pia aliwahi kushi Moshi na Iringa kikazi.Mungu Amlaze Pema Mzee Njenga Amin

No comments:

VIJANA WA TANZANIA HUENDA WAPI KUPUMZISHA AKILI BAADA YA SAA ZA KAZI?

AWALI HAPA PALIKUWA NA JENGO LILILOITWA  NYUMBA YA SANAA WASANII WENGI WALIKUWA WAKIFANYA KAZI ZAO HAPA, KWA SASA KILICHOBAKI JINA WASANII...