RayC - Rehema Chalamila

Rehema Chalamila binti mwanamuziki maarufu aliyezaliwa Mafinga, Iringa  May 15, 1982 maarufu kwa jina la  Ray C na pia kwa kiuno bila mfupa, ambae ameweza kufurahisha nyoyo za wengi kwa sauti yake tamu, kwa wakati huu inasemekana yuko katika mtihani mkubwa wa kujaribu kuacha kutumia madawa ya kulevya. Kumekuweko hadithi mbalimbali kwa muda mrefu kuwa anajihusisha na matumizi ya madawa hayo, hatimae sasa inadaiwa hali imefikia pabaya kiasi cha kulazimika kuingia kwenye hospitali zenye utaalamu wa kusaidia kuacha matumizi ya madawa hayo(Rehab). Ikiwa ni kweli wote tuliokuwa tukipenda muziki wake tumuombee Mungu ampe nguvu aweze kushinda mtihani huu mgumu

Comments