RIP Amigolasy |
KHAMIS AMIGOLAS
wanamuziki wa miaka mingi aliyepitia bendi kadhaa zikiwemo African Beat, African Stars na hatimae Ruvu Stars amefariki dunia jana usiku kutokana na
ugonjwa wa moyo ambao wanaomfahamu wanasema ulikuwa ukimsumbua kwa miaka mingi.
Khamis aliyefahamika sana kwa mustachi wake alikuwa mwanamuziki muimbaji mtulivu
na mcheshi, mwenye kupenda utani sana. Msiba uko jirani na shule ya Msingi ya Mianzini Mburahati.
Mpaka sasa jamaa wa karibu wametaarifu kuwa mazishi yatakuwa kesho Jumatatu mchana katika makaburi ya Kisutu,
Mungu ailaze pema peponi roho yake Amin
Comments