Kwa wale wapenzi wa sinema za Kinaijeria jina au sura ya Rich
Oganiru si ngeni, ila wiki chache
zilizopita alipata mkasa unaofanana sana na filamu zao. Baada ya kufiwa na mkewe na Oganiru alikamatwa kwa kosa la mauaji ya mkewe huyo, lakini kwa maelezo yake hadithi ni tofauti kabisa. Kadri ya maelezo ya Rich
mkewe aliaanza matatizo ya afya miezi mitano iliyopita akisumbuliwa na
‘fibroids’.Pamoja na mkewe kufanyiwa operesheni na daktari wa Kijerumani,
fibroid hizo ziliendelea kukua na kumsumbua mkewe. Hivyo akajaribu kumpeleka
mkewe kwa Prophet TB Joshua, wakati wanangoja kuonana nae mkewe alitoa wazo
kuwa ahamie kwenye nyumba ya kaka yake kwenye kambi ya Jeshi la anga huko
Shasha. Alipofika huko akawa anakataa chochote alicholetewa na mumewe na kuwa
anakula kile tu alichopikiwa dada yake au kuletwana kaka yake. Hali yake ikaendelea
kuwa mbaya, wakakubaliana kuhamia kwenye eneo la Sinagogi la TB Joshua kungoja
appointment, lakini mkewe tena akabadili mawazo na kuomba kupelekwa hospitali
ya Jeshi. Wakati wanampeleka wakiwa na shemeji yake, kaka wa mkewe huyo, mkewe alifariki wakiwa
kwenye geti la hospitali. Rich alipoteza fahamu kutokana kupandwa kwa presha
kwa kifo cha mkewe na kulazwa, alipozinduka, akakuta shemeji yake kishapeleka
mwili mochwari lakini akamlazimisha yeye kwenda kuwaeleza wakwe zake kuwa binti
yao kafariki. Aliomba apewe cheti cha kifo kusaidia kueleza kuhusu kifo hicho, lakini shemeji yake akawa mkali na
kumfukuza toka hapo. Aliporudi kwenye hoteli ambako alikuwa akiishi akagundua
kuwa kila kitu cha mkewe kilikuwa kimeondolewa chumbani na vitu vyake
vimepekuliwa. Anasema hata funguo za gari lake na passport yake vilichukuliwa
na akalazimika baadae kubembeleza shemeji yake amrudishie. Hatimae alipofika
nyumbani kwake akakuta pia huko vitu vyote vya mkewe vimeondolewa mpaka picha
zao za harusi. Baada ya siku tatu ndipo polisi walikuja kumweka chini ya ulinzi kwa
mauaji ya mkewe. Alipofika rumande akakuta wafungwa walio wananchama wa Boko
Haram wakawa wanamlazimisha kuwafulia nguo. Aliachiwa alipoonekana afya yake
inadorora, lakini hata hivyo baada ya siku chache polisi walikuja tena na kumzoa tena kwa kipigo kikubwa.
Rafiki yake ndie aliemsaidia kwa kulazimisha postmortem ifanywe kuona sababu za
kifo ambapo baada ya kuonekana kilikuwa kifo kutokana na ugonjwa akaachiwa.
Wakati akiwa kwenye hizi kasheshe, mke wake akazikwa bila taarifa kwake.....yaani stori kama filamu zao. Mungu amlaze pema mke wa msanii huyu
Comments