Sandton Sound bendi ambayo waimbaji wake ni wale ndugu Christian Sheggy na Francis Sheggy. Ni bendi nyingine ambayo haivumi lakini imo sana tu. Nimewakuta pale Legho Hotel Shekilango wakiporomosha muziki wa aina mbalimbali, ililazimika nishike gitaa pale walipoanza kuimba ule wimbo ambao ulikuwa utunzi wa Kyanga Songa ambao nilishiriki kupiga rythm gitaa miaka hiyo 1988/89. Masikitiko. Kwa wale wenye kumbukumbu kibwagizo chake kilikuwa
Kinachonisikitisha ni kuona kwamba nakosa mume,
Wakunioa mama,
Nami nijisikie kama wenzangu waliobahatika kuolewa
Hiyoooooo hiyooooFrancis Sheggy |
Christian Sheggy |
Hatib Said alikuwa TOT Band |
Moses Miliya alipigia SOT Sound |
George Peter aliwahi Police Jazz Band |
Manager wa Bendi Muba ni mtoto wa Mzee Muba aliyekuwa mwanamuziki wa Dar es Salaam Jazz Band. |
Mohamed Mussa aka Soso ni Bassist alikuwa mwanamuziki wa Super Matimila |
George Peter |
Comments