Aslay- na NAKUSEMEA, kipaji cha hali ya juu

Bila wasiwasi ASLAY kutoka katika kampuni  ya Mkubwa na Wanawe TMK, ana sauti yenye ukomavu kuzidi umri wake wa kimaisha ya muziki. Mwimbaji mzuri ni yule ambaye anapoimba we msikilizaji unapata hisia ya ujumbe anaoutuma. Aslay ananikumbusha sifa aliyokuwa akipewa Michael Jackson alipokuwa mdogo, alikuwa akiweza kuimba kwa hisia ambayo kwa kawaida hutokana na kupitia machungu au furaha unayoiimba. Nalisikia hilo katika sauti ya Aslay. Namuombea Mungu kijana huyu aepuke na ulevi wa aina yoyote ile ili aweze kufaidi kipaji hiki ambacho Mola amemjalia, kwani kwa sauti hii na management inayotakiwa hakuna ambacho hataweza kufanya. Mungu amjalie asidharau elimu ili aweze kutumia vizuri elimu yake kupata kila kinachostahili kutokana na kipaji chake.

Comments