Kutokana na maelezo kutoka blog mbalimbali ikiwemo Mjengwa Blog na Sundayshomary.com mwanadada muimbaji aliyekuwa kipenzi cha Watanzania mara baada ya kutoa wimbo wake Chambua kama karanga, Bi Saida Karoli amefariki dunia baada ya chombo alichokuwa akisafiria kutoka kisiwa cha Goziba kuzama baada ya kupigwa na dhoruba kubwa. Bado habari zaidi hazijapatikana hivyo tunasubiri habari za ziada na kuweza kuwapasha wapenzi wa mwanadada huyu.
Comments