Habari ambazo si nzuri kutokea wala kuandika, hatimae zimetokea, msanii Ommy Dimpoz kupitia akaunti yake ya twitter
ametweet kwamba amemkamata rapper wa Nako 2 Nako Lord Eyes akiiba vifaa
mbalimbali vya gari yake. Pamoja na mengine Ommy
aliongeza kuwa Lord amekuwa akifanya mchezo huo kwa watu wengi. Ilikuwa ikijulikana kuwa kwa muda mrefu Lord Eyes alikuwa mpenzi wa RayC ambae inadaiwa anasumbuliwa na matatizo ya madawa ya kulevya. Kuna mengi ya kujifunza kwa wasanii wengine katika habari hizi
Comments