Katika mji wa Muscat, vikundi vingi vya muziki kutoka Tanzania vimekuwa vikifika na kufanya masikani. Bendi kama Tanzanite, Kilimanjaro, InAfrika, African Stars, African Beat, na nyingi nyingine zimepita katika mji huu. Kati ya bendi ambazo zimekuwa huko kwa muda mrefu ni Jibal Band, yenye wanamuziki kama Amour Saleh Amour maarufu kama Zungu ambaye amewahi kupigia kinanda bendi za Twanga Pepeta, TOT, DoubleM, Edson Teri aliyeanza kupata umaarufu katika kile kipindi cha Bongo Star Search na kupitia Band kadhaa baada ya hapo, ikiwemo African Beat ya Mafumu Bilali, mpiga gitaa Bonzo Kwembe na wenzao, wamekuwa katika ukumbi wa hotel ya Ramee Dream wakipiga muziki karibi kila siku, wakisindikizwa na show safi ya nguvu hapa ni baadhi ya wanamuziki hao
Comments