Ili kuwezesha kufika Dodoma na kuwakilisha mapendekezo
yaliyokusanywa na Mashirikisho, Mtandao wa Wanamuziki Tanzania (TAMUNET),
waliwezesha idadi ya wasanii 12 kufika na kuishi Dodoma. Wasanii hao wakiwemo
viongozi toka Mashirikisho wameza kufika Dodoma na kuanza kazi mara moja ya
kukutana na Wabunge mbalimbali, na kufanya nao mikutano na mazungumzo ya papo
kwa popa na kwa kweli mapokezi yamekuwa ya hali ya juu yanayoleta tumaini kubwa
kwa wote waliofika huku. Wasanii
waliomo katika msafara huu muhimu kwa tasnia na Taifa ni
1.
Simon Mwakifwamba – Rais, Shirikisho la Filamu
(TAFF)
2.
John Kitime – Mwenyekiti, Tanzania Musicians
Network (TAMUNET)
3.
Bishop Hiluka – Katibu Mkuu, TAFF
4.
Yobnesh ‘Batuli’ Yusuph –Msanii/FilmProducer
5.
Samwel ‘Braton’ Mbwana –Tanzania Urban Music
Association (TUMA)/Music Producer
6.
Paul ‘P Funk’ Matthysse – Mwenyekiti, Tanzania
Producers Association/ Producer
7.
Kulwa ‘Dude’ Kikumba – Msanii/ Producer
8.
Abdul Salvador –Katibu Mkuu, Shirikisho la
Muziki Tanzania (TMF)
9.
Adrian Nyangamale – Rais, _Shirikisho la Sanaa
za Ufundi Tanzania
10. Mh.
Paulynus Raymond Mtendah – Mbunge Bunge la katiba
11. Yvonne
Cherie ‘Mona Lisa’ –Msanii
12. Seleman
Hamisi- Producer toka Dodoma
13. Ernest
Omalla – Mshauri wa TAFF na TAMUNET
Mara baada ya kufika Dodoma Mbunge wa Bunge la Katiba Mh.
Maria Sarungi aliwezesha kufanyika kikao cha kwanza kati yake na wasanii ambapo
pia Mh. Paul Makonda alikuweko. Mazungumzo yalifanyika ambapo msafara ukaweza
kueleza mapendekezo yake kupitia mshauri mtaalam Ernest Omalla na mwanamuziki
John Kitime. Mkutano huu wa saa mbili ulikuwa wenye matumaini makubwa.
Msafara
ulitoka hapa na kwenda kwenye mkutano mwingine ambapo msafara tena ulitoa
maelekezo yake kwa waheshimia Wabunge watatu, Mh Paul Mtanda, Mh.Livingstone na
Mh Murtaza Mangungu, na tena mkutano huo ulikuwa ni mzuri wenye mafanikio
mazuri sana. Mheshimiwa Mtanda aliahidi atajitahidi kukusanya wajumbe wa kamati
ya Ustawi wa Jamii ili kuweza kupata uelewa wa maombi ya wasanii.
Kamati haikuishia hapo kwani jioni Mheshimiwa Makonda aliiwezesha kundi hili kukutana
na wabunge wengine wakiwemo Mh.
Ahmed Salum, Mh. William Mgeja na Mh. Mpina Mbunge wa Kisesa.
Katika hali ya
kuonyesha kuwajali wasanii wabunge wa Dar es Salaam waliwafuata wasanii katika
Lodge waliofikia na kuwasikiliza lile ambalo walikuwa wakilitaka. Mheshimiwa
Idd Azan na Mh. Abbas Mtemvu waliwakilisha wabunge wa Dar es Salaam na kuwa na
saa nzima ya kuwasikiliza wasanii hawa katika malengo yao
mawili waliyotaka yaingie katika Katiba.
Comments