Kamati ilipata
mapokezi ya heshima kubwa kutoka kwa wabunge wa CHADEMA, ambapo Wabunge sita wa CHADEMA walikaa na kuwasikiliza
wawakilishi hawa wa wasanii wakieleza mapendekezo yao katika Katiba kuhusiana
na wasanii. Wasanii wana ajenda mbili,
1. Kundi la wasanii kutajwa katika
Katiba kuwa ni kundi rasmi kutokana na ukubwa wa kundi hili nchini, kama yalivyotajwa makundi ya wakulima, wafugaji, wavuvi na kadhalika, pia mchango
wake katika ajira ya vijana na ukubwa wa pato linalotokana na kundi hili,
ambalo kutokana na kutokutambuliwa linapotea katika mifuko ya watu na kukosesha
wasanii na Taifa pato kubwa.
2. Wasanii walitaka ubunifu ulindwe kwanza kwa
ulinzi wa Milikibunifu kutajwa rasmi katika katiba na hivyo kuwezesha sheria bora kutungwa na pia
utekelezaji wa ulinzi wa kazi zao uweko kama ilivyo katika mali nyingine za
wananchi wengine. Kikao cha saa moja na nusu kilikuwa cha mafanikio na kuwa na
faida kwa pande zote mbili.
Wasanii hawakulala mapema kwani walimalizia siku na
kuhamia eneo jingine ambapo
walikuwa na kikao na Mheshimiwa Mbunge wa Donge ambae pia ni Mwenyekiti wa
Ummoja wa Vijana wa CCM Taifa Mheshimiwa Sadifa, ambapo kikao hicho kiliisha saa saba
ya usiku.
Comments