Semina ya TRA ya URASIMISHAJI WA TASNIA YA MUZIKI NA FILAMU,
imeisha kwa kusambaratika bila kuagana rasmi kutokana na wasanii kuja juu
na kuuliza maswali ambayo majibu yake hayakuwaridhisha wasanii.Hivyo kuzuka mtaafaruku mkubwa katika ukumbi.
Semina hiyo ambayo ilitangazwa kuwa ingekuwepo katika ukumbi
mkubwa wa Jumba la Makumbusho ya Taifa katikati ya Jiji la Dar es salaam
ilikuwa imepangwa ianze saa nne lakini ilichelewa na kuanza saa 5. Wasanii mbalimbali, vijana na wazee wa
filamu na muziki wakisindikizwa na viongozi wa vyama na Mashirikisho yao
walikuwemo. Kwa upande wa serikali kulikuweko na Maafisa kutoka Ukurugenzi wa
Utamaduni, BASATA, COSOTA, Bodi ya Filamu wakiongozwa na TRA ambao ndio walikuwa wasemaji wakuu. Semina ilianza kwa
maelekezo kuhusu nini kitakachofanyika ili kuanza kuhakikisha stika za TRA
zimebandikwa kwenye kila kazi ya sanaa(CD,DVD,Kanda na kadhalika). Kwa maelezo ya muwezeshaji hili lingeleta
faida kwa kulinda haki za wasanii. Iliilezwa kuwa taratibu hizi zitaanza Januari 2013 kwa kazi
zote mpya na kwa kazi ambazo ziko dukani zitatakiwa zote kuwa na stika hizo
kufikia July 2013. Kazi zote
zilizotakiwa kusambazwa nchini kuanzia sasa, zingelazimika kupitia COSOTA, BASATA, na
Bodi ya filamu kabla ya kuruhusiwa kupewa stika. COSOTA itakuwa ikihakikisha uhalali wa kazi,
BASATA na Bodi ya filamu kuhakiki maadili ya kazi husika.Wasanii waliporuhusiwa
kuuliza maswali walihoji kwanza kuhusu zilipofikia Kanuni za sheria ya filamu,
kwani ni muhimu katika taratibu hizi, na pia wasanii walihoji COSOTA ina muwakilisha nani?, kwani
ilikwishabadilika kinyemela kutoka kuwa Chama cha wenye Hakimiliki na kugeuzwa
kuwa kitengo cha serikali, na kuanzia 2007 hakijawahi kuitisha mkutano na wadau,
japo kinaendelea kukusanya fedha za wadau. Wasanii pia waliuliza TRA kwanini
inadai inawalinda wasanii wakati ni wazi katika hili kazi yake itakuwa ni
kukusanya kodi kutoka kwa wasambazaji, jambo ambalo halina tija yoyote kwa
wasanii binafsi. Majibu yaliyotolewa yalileta mvurugano kiasi cha kusababisha
viongozi wote kuondoka kimyakimya kupitia mlango wa nyuma na kuwaacha wasanii
wakiendelea na kikao kisicho rasmi ambacho kilihamia nje ya kufikia kutengeneza kamati ambayo
itatayarisha mkutano mkubwa wa wasanii wote wa muziki na filamu kutoa tamko la
pamoja.Tatizo la taratibu hizi zinazotaka kuanzishwa hapa nchini ni
mpya kabisa hazijawahi kufanyika nchi nyingine yoyote kwa mtindo huu, haieleweki
kwanini serikali inataka kugundua njia ya kibongobongo ya kulinda kazi za wasanii, wakati duniani kote
taratibu zinafahamika, hii inaleta picha kuwa serikali inahitaji tu kodi kutoka
kwa wasanii lakini haina mpango wa dhati kuhusu wasanii.
|
Maswaliiii |
|
Wasanii nje ya ukumbi mkutano ukiwa unaendelea ndani |
|
Mkutano wahamia nje |
Comments
wamekurupuka!