Madansa wa Tanzania ambao ni maarufu kwa jina la ‘ wacheza
show’ hatimae wameweza kuunda chama chao Tanzania Dancers Association, ambacho si tu kina uongozi wa Kitaifa
lakini pia tayari kina matawi ya kiwilaya. Jambo ambalo vyama vingi vya sanaa
havijaweza kufikia.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hiki ni Bi Husna Katibu wake akiwa ni dansa maarufu Chino Loketo.
Viongozi wa Taifa |
Jumatatu hii chama hiki kilifanya mkutano mkubwa na
kumkaribisha Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki kuwa mgeni rasmi wa
mkutano wao huu mkubwa uliofanyika pale Garden Breeze Magomeni.
Pamoja na John Kitime pia walialikwa wanamuziki maarufu kama
Waziri Ally wa Kilimanjaro Band, Nyosi El Saadat Rais wa FM Academia, Ally
Chocky Mkurugenzi wa Extra Bongo, na Hussein Tendega maarufu kama Hussein
Macheni.
Katika kikao hiki, Nyoshi alitoa mchango wake kwa chama wa
shilingi laki moja, na Ally Choky aliahidi laki mbili, Hussein Macheni pia
aliahidi laki mbili. Hussein Macheni amekuwa kiungo kikubwa kwa madansa hawa
kwa kuwa wakati akiendesha bar maarufu kwa jina la Macheni madansa wengi
walipitia katika ukumbi wake.
Mgeni rasmi aliwasifu madansa kwa kuanzisha chama chao, na pia alitoa msaada wa kuwaboreshea Katiba yao na kuwaahidi kuwaunganisha na vyama
vingine vya madansa nje ya mipaka ya Tanzania.
Madansa walionyesha uwezo wao kwa kufanya show mbalimbali
kama zinavyoonkana katika picha na video hapa chini
Nyoshi El Sadat |
Ally Chocky |
Waziri Ally |
Hussein Macheni akihutubia |
Comments