Kati ya vikundi vilivyokuwa ni tishio katika Taarab kwenye miaka ya 90, kundi la TOT lililo chini ya Chama Cha Mapinduzi, lilikuwa mojawapo, naweza kudiriki kusema liliweza hata kuwa ndilo kundi lililopendwa zaidi na wapenzi wa Taarab wakati huo. Likiwa na mpambano mkali na kundi la Muungano Cultural Troupe, na hatimae kubaki peke yake baada ya kundi la Muungano kumeguka, jambo ambalo huwa linasadikiwa lilichochewa na uongozi wa TOT; TOT bado iko hewani na bado ina washabiki wengi. Juzi nililikuta kundi hili likiwa hewani katika ukumbi wa Copacabana Mwananyamala. Na pia kulikuweko na wanamuziki wengine wengi kutoka vikundi vingine vya Taarab hapa mjini.
Malkia Bi Khadija Omar Kopa |
Show siku hizi ni sehemu ya Taarab |
Binti ya Mwanamtama ambae yuko East African Melody |
Mwanamtama aka Mama Lao |
Bi Aisha alikuwepo aliimba wimbo wake wa Mama |
Thabit |
Comments