Nilipatwa
na mshangao mkubwa baada ya kukumbuka jambo lililosahaulika na pengine
kutofahamika kwa wengi la marehemu Isiaka Gobby linalofanana sana na tukio la
Steven Kanumba
Hatua
chache baada ukiingia katika lango la makaburi ya Kinondoni, kushoto kwako
utalikuta kaburi la msanii Steven Kanumba. Kanumba akiwa na umri mdogo wa miaka
28, alifariki ghafla katika mazingira ambayo yamepelekea msanii mwenzie Elizabeth Michael kuwa katika kesi ya
kutuhumiwa mauaji ya msanii huyu aliyekuwa mahiri katika kazi yake ya usanii wa
kuigiza na pia aliyekuwa na sura ya kupendeza yenye mvuto, wengi tunamfahamu kwani
bado yuko katika mawazo yetu kutokana na kazi zake kuwa bado zikiendelea
kuonekana katika vyombo mbalimbali vya utangazaji. Jirani kabisa ya kaburi la
Kanumba, kuna kaburi moja la zamani sana la mwanamuziki Isihaka Gobyy. huyu alikuwa mwanamuziki wa Orchestra
Makassy katika miaka ya 1976/77. Gobby nae alikuwa na sifa zilizofanana sana na
zile za Kanumba. Kwanza alikuwa mwanamuziki muimbaji mahiri sana, pili alikuwa
na sura yenye kuvutia sana.
Wakati huo bendi ya Makassy ikiwa na
makao makuu ukumbi wa Hunters, ikiwa na ushindani mkubwa kutoka kwa bendi ya
Bana Ngenge iliyokuwa katika
ukumbi mwingine jirani wa Savannah, na Orchestra Maquis du Zaire iliyokuwa
ikipiga katika ukumbi wa Resort Kimara.
Gobby
nae alikufa kifo cha ghafla akiwa na miaka 28, kwa kuuwawa kwa kupigwa na
hatimae kuchinjwa kama kuku katika ugomvi uliovuma wakati huo kuwa ulikuwa
ukihusu mapenzi. Hakuna taarifa za kuwahi kukamatwa aliyemfanyia Gobby unyama
huu uliopoteza maisha yake mwanamuziki huyu kijana.
Mungu awalaze Kanumba na Gobby Pema Peponi
Comments