UNAIJUA DOUBLE A MUSICA?


BENDI inayoongozwa na mkung’utaji tumba wa zamani wa Mlimani Park Sikinde, Abbas Abdallah, Double A Musica, jana alitimua vumbi zito la burudani, kwenye ukumbi wa Taxido, Buza Kanisani, jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa habari hizi alikuwapo ndani ya ukumbi huo wakati bendi hiyo ikifanya mambo yake na kushuhudia namna mashabiki walivyokuwa wakijimwaga katikati kwa wingi kucheza pamoja na kutuza baadhi ya wanamuziki walioonekana kuwavutia zaidi.
Mbali na kutumbuiza vibao vya kukopi, bendi hiyo pia ilipagawisha mashabiki kwa vibao vyao wenyewe ambavyo navyo vilionekana kukonga vilivyo nafsi za mashabiki waliokuwa wamehudhuria.

Comments