EXTRA BONGO NDANI YA UKUMBI WA FLAMINGO MAGOMENI MWEMBECHAI

ALLY Choki ‘Mzee wa Kijiko’ juzijuzi alikuwa ndani ya ukumbi wa Flamingo, Magomeni Mwembechai akimwaga burudani ya aina yake kwa mashabiki wake wa Kinondoni, hususan wakazi wa eneo hilo.
Muziki ulikuwa wa kutakata sana, ambapo wanamuziki wote wa bendi hiyo walionekana kujituma kikamilifu jukwaani na kuifanya shoo iwe tamu masikioni na machoni mwa waliohudhuria.
Lakini hata hivyo, dosari mbili tatu hazikukosekana, baadhi yake ikiwa ni kama vile Choki mwenyewe kulikimbia jukwaa na kuwaachia ‘madogo’ kwa muda mrefu.
Kadhalika, kana kwamba aliyekuwa akimuiga Choki, nguli Banza Stone naye alitumia muda mwingi kitini kuliko jukwaani na hiyo kuwafanya mashabiki waboleke kwa kiasi fulani.
Hata zilipopigwa baadhi ya nyimbo ambazo nao wameimba kwa kiasi kikubwa, mastaa hao hawakuonekana kabisa jukwaani na hivyo mapengo yao kuzibwa na waimbaji Bob Kisa na Athanas Montanabe.
Ukiondoa hiyo mambo yalikuwa mazuri siku ya jana kwa wapenzi na mashabiki wa waliopata fursa ya kuhudhuria shoo hiyo ambayo kiingilio chake kilikuwa ni kinywaji.








Comments