MISS SAN DIEGO KUPATIKANA JUMAPILI HII, TANDIKAKILE kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa San Diego Pub ‘Miss San Diego’ kinatarajiwa kufika kilele Jumapili hii, kwenye ukumbi wa Sun Diego, Tandika, jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Viumbe Wazito Promotion ambao ndio waandaaji wa kinyang’anyiro hicho wakishirikiana na San Diego Pub, Edson Ketto, ‘Mzee wa Channel Ten’ alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa, jumla ya vimwana 10 watapanda jukwaani kuchuana siku hiyo.
Ketto alisema kuwa, kinyang’anyoro hicho kitapambwa na burudani kemkemu kutoka kwa wasanii wa Taarab na Bongofleva, wakiwamo Jokha Kassim, Dogo Mfaume, Inspekta Haroun na Ashura Machupa.
Ketto aliwaomba mashabiki pamoja na wapenzi wa tasnia ya urembo hapa nchini, kujitokeza kwa wingi, ili kushuhudia laivu kisura atakayetwaa taji hilo la Miss San Diego kwa mwaka huu.

Comments