Skip to main content

UNATAKA KUSHIRIKI TUZO ZA MUZIKI ZA AFRIMA?

-->
Watayarishaji wa tuzo za All Africa Music Awards (AFRIMA) wamezindua uandikishaji wa watakaowania tuzo za AFRIMA kwa mwaka 2016. Wanaotaka kushiriki katika tuzo hizi wanatakiwa wawe wametuma maombi ifikapo tarehe 30 July 2016. Hii ni mara ya tatu kwa tuzo hizo kutolewa na kuna ‘category’ mbalimbali zitakazoshindaniwa. Mwaka huu shughuli za utoaji wa tuzo hizo utafanyika nchini Gambia, baada ya kufanyika Nigeria kwa mara mbili zilizopita. Tuzo hizo zimekwisha pata baraka ya Umoja wa Afrika (AU) hasa baada ya Angela Martins, Mkuu wa Idara ya Utamaduni ya Umoja wa nchi za Kiafrika kutamka wakati wakati wa uzinduzi wa tuzo hizi kuwa umoja huo utaendelea kukuza mahusiano ya nchi mbalimbalikwa kutumia  tasnia ya ubunifu katika kazi za muziki, na  kwa kuunganisha shughuli hizi katika matamko ya Charter for African Cultural Renaissance, African Youth Charter  na AU Plan of Action on Cultural and creative industries. Mike Dada, Rais na Executive Producer wa AFRIMA, amewaomba wasanii, mameneja, maproducer, wenye record labels, na maajent kuwahi kuwasilisha maombi ya wasanii wao. Alionya kuwa hata msanii akiwa maarufu namna gani AFRMA haitapokea kazi zilizochelewa kuwasilishwa, na wala AFRIMA haitawafuata wasanii popote. Tarehe ya kuanza kuwapigia kura wasanii itakuwa tarehe 26 Agosti 2016, na AFRIMA Academy itaanza kupitisha majina tarehe 26 Septemba 2016, na shughuli ya kutafuta washindi itaisha tarehe 5 Novemba 2016.
Kwa mwaka jana tuzo hizi ziliwawezesha Diamond Platnumz, Charlote Dipanda kupata tuzo tatu kila mmoja, washindi wengine walikuwa Stanley Enow na Olamide Ukitaka kushiriki ingia hapa


Comments

Hammer Q said…
Asante sn tunapoelekea pazuri

Popular posts from this blog

Unataka kujifunza muziki?

Je ungependa kujua Kurekodi muziki, Kusoma Muziki, Kuandika Muziki, Kuimba na Kupiga Ala mbalimbali za kisasa za muziki ? Kama ndivyo, basi waone AlphaBeta Music Centre waliopo TABATA Liwiti mkabala na shule ya msingi au wasiliana nao kwa simu +255 754 77 66 40 au +255 784 737 216. Usiikose fursa hii!!!!!

TWANGA PEPETA, NGUZA VIKING, PAPII KOCHA JUKWAANI TAMASHA LA WAFUNGWA

Bendi ya African Stars, maarufu kwa jina la Twanga Pepeta kesho itashiriki katika Tamasha la Wafungwa ambalo litaanza saa 2 asubuhi. Katika mambo ambayo yatakuwa makubwa kimuziki ni kushiriki kwa mwanamuziki mkongweNguza Viking na mwanae Papii Kocha ambao kwa sasa wanatumikia kifungo cha maish katika gereza la Ukonga. Pia katika tamasha hilo atakuweko msanii nyita wa muziki wa Singeli Msaga Sumu. Lengo la tamasha hilo ni kuwatia moyo wafungwa na kuwaonyesha kuwa wapo pamoja na Watanzania wenzao walio nje ya magereza. Eric Shigongo Mkurugenzi mkuu wa Global Publishersambao ndio walioandaa tamasha amesema hii ni mara ya pili kuandaa tamasha la namna hii, ambalo lengo ni kunyanyua ari ya wafungwa. Wafungwa waliohudhuria tamasha lililopita ambao walikwisha maliza kifungo wamesifu na kusema tamasha lililopita liliwapa faraja sana. Mratibu wa tamasha hilo Juma Mbizo, amesema mbali na burudani kali kutoka kwa Twanga, kutakuwepo na michezo mbalimbali kama ya mpira wa miguu, kuvuta kamba na mi…

RATIBA YA MSIBA WA MAREHEMU SALOME KIWAYA

Taarifa ya ratiba ya msiba wa marehemu Salome Kiwaya aliyekuwa Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma na mwanamuziki, aliyefariki jana 07/10/2016, kwa ajali ya gari maeneo ya Kilimo Kwanza Dodoma Mjini. Msiba uko nyumbani kwa marehemu Mtaa wa Image, Kata ya Kilimani, Wilaya ya Dodoma Mjini. RATIBA:
1.Tarehe 08/10/2016 - maombolezo  yanaendelea nyumbani Image Kilimani Dodoma.
2.Tarehe 09/10/2016 kuanzia saa 2:00 asubuhi - mwili wa marehemu utaletwa nyumbani kutokachumba cha maiti cha General Hospital Dodoma.
3. Tarehe 09/10/2016 saa kuanzia 6:00 mchana -salamu mbalimbali za Viongozi na Makundi Maalumu zitaanza kutolewa.
Saa 8: 00 mchana- mwili wa marehemu utatolewa nyumbani, na kuelekea Kanisa Kuu Roman Catholic. Baada ya Misa, msafara wa mwili wa marehemu utaelekea Kijiji cha Mtila, Kata ya Matola Mkoa wa Njombe kwa ajili ya maziko tarehe 10/10/2016 siku ya Jumatatu.