Walugulu
Original, ndivyo inavyojiiita bendi ya GFC Musica. Bendi hii niliikuta ikiwa
kazini katika ukumbi wa Chilakale baada ya kuelekezwa na rafiki zangu wa Facebook kuhusu kazi nzuri wanayoifanya, ni wazi pamoja na upya wa Bendi hii ikiwa
watashikilia miiko ya ujenzi mzuri wa bendi hakuna sababu kwanini wasiweze kuwa
katika bendi maarufu Tanzania, na kuirudisha Morogoro kwenye nafasi yake katika
uwanda wa muziki wa dansi Tanzania.
Bendi
nyingi zimechukua mfumo wa muziki wa Kikongo wa kupiga sebene na pia kuwa na
wacheza show wengi na hivi ndivyo ilivyo kwa bendi hii. Kwa hiyo imeingia
katika mashindano ya kutafuta nafasi ya kung’ara katika mtindo huo, kwa vile
bendi ina vyombo vipya vizuri, wanamuziki wachanga wanaoonekana wana ari ya
kufanya kazi, na pia wana mlezi ambaye ana nia ya kuona bendi inapata
mafanikio, na pia kwa vile wasanii wanauwezo mkubwa, hakuna sababu yoyote
kwanini hawataweza kuleta upinzani kwa bendi kubwa ambazo zimekwisha ota mizizi
kama, Twanga Pepeta, Extra Bongo na kadhalika.
Comments