The International African Festival Tubingen




The International African Festival Tubingen, ambalo kwa sasa linajulikana kama “AfricActiv” limetimiza  toleo la 3. Na katika onyesho la mwisho magazeti ya Tubingen yanakisia kuwa watu 15,000 walihudhuria  Tamasha hili.
CEO na muasisi wa Tamasha hili Bi Susan Tatah alisema Tamasha hili litakuwa ndio Tamasha kubwa la muziki wa Kiafrika katika Ulaya. Mwaka  huu kumekuweko na watu waliotoka moja kwa moja toka Afrika kutoka nchi kama Burkina Faso, Mali na Kenya kwa ajili ya Tamasha hili, na kulikuweko na Bloggers zaidi ya milioni 25 kutoka Afrika hasa Afrika ya Mashariki waliyoongelea na kufuatilia shughuli za Tamasha hili. Tamasha hili lilionyesha Afrika ni nzuri na ina mengi yenye utamu wa  asili
 Katika Tamasha hili Bendi ya Ngoma Africa chini ya uongozi wa Ibrahim Makunja iliweza kupata International Diaspora Award kama moja ya vikundi vilivyofanya kazi nzuri katika Tamasha hili. Bi Susana aliomba vikundi vianze kujisajili kwa ajili ya kushiriki tamasha hili 2013, litakalofanyika kuanzia tarehe 8 hadi 11 August 2013

Comments

Anonymous said…
It is not my first time to visit this web page, i am visiting this web page dailly and
obtain fastidious information from here all the time.
Here is my weblog ; car donation tips