Leo imekuwa siku ya kuzunguka katika sehemu mbalimbali, nilianzia Sinza katika Bar ya T Garden ambapo kulikuweko na bendi inayoongozwa na mpiga bezi wa zamani wa Sikinde Mzee Julius Mzelu- JM MBETA BAND
|
Fred Mzelu |
|
Julius Mzelu |
Nikatoka hapo na kuenda kuangalia mashindano ya Miss Ilala, sikukaa sana maana kwa kweli vyombo vilivyotumika kwa sauti viliipunguza utamu show ile, niliona alfu ishirini yangu imeenda kama sadaka. Nikapita Mango Garden ambako niliwakuta Akudo Band wakiwa na muimbaji wao mpya anayejitambulisha kwa jina la 'Lialia'
Hatimae nikapita Mashujaa muzika na kumkuta Charlz Baba na kundi lake katika ukumbi wa Business maeneo ya Victoria
Comments