Nimekwenda
gereza la Ukonga asubuhi hii kumsalimia Nguza na mwanae Papii, nimewakuta
wachangamfu wenye afya nzuri. Nguza kanituma NIWASALIMIE WOTE, naomba nitumie
jukwaa hili kutangaza salamu hizo. Ni wazi italazimika kuomba muda wa ziada
kutoka kwa uongozi wa Magereza kuzungumza zaidi na Nguza, jambo mojawapo ambalo
tutalizungumza ni kuhusu mapato ya wimbo wa Seya. Pamoja na umaarufu wote ni
jambo la kusikitisha kuwa Nguza anasema hajapata fedha yoyote kutoka wimbo ule,
zaidi ya fedha alizopewa kuingia studio kuurekodi. Swali ni nani anazipokea
fedha za wimbo ule?
Comments