Mchoraji Ramón Esono Ebalé |
Cartoonists Rights Network International (CRNI) imemchagua mchora vibonzo.
Ramón Esono Ebalé ambaye kwa sasa yuko
kizuizini Equatorial Guinea kuwa mshindi wa tuzo la ’2017 Courage in Cartooning Award.’
CRNI kimesema kuwa
kuchaguliwa kwa Ramon kumetokana na ‘Kuendelea kwake kukataa kutishwa , na
ujasiri wake dhidi ya selikali dhalimu’.
Joel
Pett, Rais wa Bodi ya wakurugenzi ya ya CRNI alisema ‘ Ramón Esono Ebalé ni mzaliwa
wa Equatorial Guinea ambaye kwa muda mrefu alikuwa akiishii Paraguay,’
Tuzo la ujasiri la Award
for Courage in Editorial Cartooning ni kengele ya kila mwaka inayotolewa kwa
wachora vibonzo walioonyesha ujasiri na kujitoa katika kuendeleza fani yao
na kutetea uhuru wa kujieleza.
Ramon alikamatwa tarehe 16 Septemba 2017 na vyombo vya usalama katika
mji wa Malabo mji mkuu wa Equatorial Guinea. Kama ilivyosemwa hapo awali, Ramon alikuwa anaishi nje ya nchi na
alikuwa karudi kwao kupata hati mpya ya kusafiria. Picha za mchoraji huyu mara
nyingi zilikuwa zikimuongelea Rais na watumishi wengine wa serikali, kulikuwa
na wasi wasi kuwa akikamatwa atashtakiwa kwa kosa la kukashifu viongozi, lakini
amefunguliwa mashtaka ya kutakatisha pesa. Makosa ambayo CRNI inadai ni ya
kutunga.
Tuzo lilikabidhiwa kwa Ramon japo kuwa hakuweko, wakati wa mkutano
mkuu wa Association of American Editorial Cartoonists, uliofanyika siku ya
tarehe 4 Novemba 2017 Hofstra University campus, Long Island, New York. Tayari maelfu ya watu wamekwisha tia saini maombi ya kuachiwa kwake, na hasa
wakidai kuwa sheria ya nchi hiyo
hairuhusu mtu kuwekwa kizuizini zaidi ya masaa 72 kabla hajafunguliwa mashtaka.
Mashirika ya kupigania haki za binadamu ya International rights group na Human
Rights Watch (HRW)
yamejaribu kuwasiliana na Rais wa nchi hiyo President Teodoro Obiang Nguema, kumuomba kumuachia mchora vibonzo huyo na kufuata matakwa ya sheria ya nchi hiyo.
Comments