Hakimu
Devotha Kisoka wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo ametupilia mbali kesi
iliyofunguliwa na Hamisa Mabeto dhidi ya mwimbaji mashuhuri Diamond Platnumz. Hamisa alifungua kesi ambayo
pamoja na mambo mengine alikuwa akiomba matunzo ya mtoto waliyezaa pamoja na
muimbaji huyo. Hamisa alikuwa akiiomba mahakama imuamuru muimbaji huyo pamoja
na mambo mengine atoe matunzo ya milioni tano kwa ajili ya mtoto.
Katika hati
ya majibu kinzani, Diamond alieleza kuwa maombi ya matunzo ya mtoto ya shilingi milioni tano kwa mwezi ni makubwa
mno hawezi kuyamudu.
Comments