Mara baada ya kumaliza kushiriki kuigiza kwa mara ya kwanza katika
katika tamthiliya ya MTV, inayoitwa
SHUGA,Vanessa Mdee ameachia wimbo wake mpya unaoitwa Kisela. Katika tamthiliya
hiyo ya SHUGA, Vanessa ameshirikiana na waigizaji wa Afrika Kusini kama Nick Mutuma and
Emmanuel Ikubese. Na katika wimbo huo mpya Vanessa ameshirikiana na
Mfalme wa Pop wa Nigeria Mr P au
Peter Okoye wa PSquare, hakika ni mambo ya kusifika. Wimbo huu wenye vyombo vya upepo vya nguvu, unaongelea
hadithi ya mwanamke analalamika anavyotendwa na mpenzi wake, anaeendesha mapenza Kisela, Producer wa wimbo huu ni Mnaijeria producer EKelly,
ambaye ana nyimbo nyingi ambazo zimefanya vizuri sana Afrika, producer huyu ndie
aliutengeneza wimbo wa VeeMoney wa Cash Madame. Video ya wimbo imeongozwa na Clarence
Peters, na hakika Peter Okoye na Vanessa wameonyesha ukomavu wao katika sana, na kazi
hii inaonyesha hasa kwanini wao ni Mastaa.
Vanessa alimsifia Peter kwa kuonyesha hasa nini maana mwanamuziki ambaye ni star , na anaona kama ni
ndoto ilikuja kuwa kweli kushirikiana naye, pia alisifu kuwa Peter amempa sio tu somo katika muziki na utoaji wa
burudani, lakini pia somo la umahiri katika kazi na unyenyekevu kwa wengine.
Comments