AWALI HAPA PALIKUWA NA JENGO LILILOITWA NYUMBA YA SANAA WASANII WENGI WALIKUWA WAKIFANYA KAZI ZAO HAPA, KWA SASA KILICHOBAKI JINA WASANII HAWATAKIWI HAPA |
NILISAMBAZA UJUMBE HUU ASUBUHI TAREHE
23JUNE 2017, BAADA YA MASAA KADHAA WATU MBALIMBALI WAMECHANGIA .........
Je vijana wa Tanzania huenda wapi
kupumzisha akili zao baada ya kazi? Hili swali bahati mbaya sana halimo katika
ajenda ya viongozi wa Tanzania, hata wale viongozi wa makundi ya vijana. Hakuna
anaewaza kubuni miradi ya kutengeneza sehemu za aina hiyo, hata viwanja au
majengo ambayo viongozi wa zamani waliyaweka kwa shughuli hizo 'social
centers', viongozi wa sasa wanazivunja na kuporomosha majengo ambayo wao huita
miradi na kusahau kabisa kuwa vijana wanastahili kuwa na maeneo ya kupumzisha
akili. Ziko wapi social halls zilioachwa na akina Joseph Nyerere? Ziko wapi
community centers zilizoachwa na wakoloni? Matokeo ya dhambi hii ni vijana
kuishia kukutana katika kumbi za bar na vijiwe visivyo rasmi. Hahihitaji akili
nyingi kujua kuwa mazoea ya kufika katika maeneo ya aina hiyo huzalisha mapenzi
ya ulevi wa pombe na hatimae dawa za kulevya. Na hakika kukosekana kwa burudani
mbadala huishia vijana kuona burudani nyingine pekee ni ngono. Sikiliza tungo
za nyimbo na hadithi za vijana wa leo, angalia video na filamu asilimia
kubwa ni kutukuza pombe na ngono. Uvaaji
na uchezaji wa mabinti ni wa kuelekeza kuwaza ngono, si ajabu kukuta moja ya
biashara zinazolipa ni guest houses. Utumiaji mkubwa wa dawa za kulevya ni
matokeo ya kukosekana sehemu halali za vijana kukutana kupeana mawazo bora.
Tulikomboe Taifa la kesho kwa kuhakikisha si kuhamasisha viwanja vya michezo
tu, pia maeneo ya shughuli nyingine za kijamii za vijana. Si kila kijana
anapenda au anajua kucheza mpira, hivyo kuhamasisha kutenga viwanja vya michezo tu hakika haitoshi.
John Kitime
FEEDBACK
1. Shukran kwa neno zuri
2. Vizuri sana mzee Kitime,
kilichosababisha yote hayo ni umiminisaition, mdudu ambaye anaendelea
kututafuna hadi sasa
3. Community Centers,zilijengwa na
Mkoloni. Baada ya Azimio la Arusha mwaka 1967. Kufuatia Sensa kubwa ya kuhesabu
Watu. Ikagundulika kuwa. Watanzania tumeongezeka sana. Hivyo mahitaji ya Tiba yakaongezeka kuliko
Uwezo wetu wa kujenga hospitali. Ndipo ikaamuriwa Community Center ya Magomeni
igeuzwe Hospitali. Ikafuatia ya Temeke. Ikajengwa Amana Hosp. Jirani ya Ukumbi
wa Kijamii wa Amana. Weneyeji maeneo ya Mnazi mmoja ambayo ndiyo kata ya
Mchafukoge kama sikosei walikutana
Anatouglou Hall. Jirani ya ilipo Amtubhai Hosp na Mnazi mmoja Hosp. Wenyeji wa
Mitaa ya Jangwani walikutana Banda la Madobi ilpoimba pia Bendi ya Kilwa Jazz.
Msimbazi/Morogoro Road. Ulikuwepo Ukumbi wa Tanzania Legions Uliotumiwa na
Mashujaa wa Vita kuu ya Kwanza na ya pili. Umeuzwa juzijuzi na Watoto aidha
Wajukuu wao!
4. Nimeona nchi kama ivory coast, Congo
rd,zina kumbi maalum Nzuri za muziki
live kama vile Zenith uliopo Paris Ufaransa na sio ktk bar kama ilivyohapa
kwetu,kuna mamia wasioenda ktk muziki
ama kujihusisha nao sababu ya mazingira yaliyopo hv sasa
5. Kweli kabisa mkuu.Huku kwetu Kenya
uko vivyo hivyo.Vijana hawashughulikiwi.Mambo yamebaki tuu ulevi,ngono,madawa
ya kulevya na uhalifu.Its very sad indeed.
6. mijini kulitengwa
maeneo ya wazi kwaajili ya michezo ambayo sasa yamechukulkwa na wenye fedha kwaajili ya faida binafsi, mikoani kila wilaya ilikuwa na ukumbi wa
utamaduni ambao sasa kumbi hizo
hakuna, mkuu kitime
umeona mbali sana
7. Kumbi nyingine zimekuwa totoro had
sasa wameona bora wageuze nyumba za ibada, mfn ddc pale morogoro
8. Kilikua Kiwanja Changu Sana,
tukishihudia vikundi kama Muungano, Mandela nk. Nikiwashuhidia watu kama Kuntu
wa Kuntu, alikua Densa Mbilikimo, Chimbende km sijakosea,
Chidumule na Dr Remmy (R.I.P) na
HAMISA wao.
Nk
9. Upo ukumbi wa juwata nao, umepoa
kbs
10. Tanga Makorora Community Centre
Ipo. Kama ni Gari, inatembelea RIM.
Kisosora Upo pia, nao halikadhalika.
Nadhani Kumbi Hizi zingetumika kama ule wa AMANA kungekua walau na faida kwa
vijana
11. Mawazo mazuri, binafsi naona ni
kutokana na wataalamu wetu wabaosimamia sheria sijui ni kujisahau au ni vipi,
maana hata miji mipya inayoanzishwa haiwi na mipango hiyo,, nikisema Wataalam
wetu namaanisha kwamba Sera na mipango inaeleza vizuri juu ya kubakisha sehemu
za social intertiment lakini haziwezi hata sehemu zao za Leaders club pia
wameziua
12. zamani walikua wakijenga hizi
community center na social halls kwa Halmashauri nyingi lkn kwa sasa hamna na
zikizopo hazina hadhi tena kulingana na wakati
13. yaan kwa sasa kimtazamo wangu, km
wizara husika, ikiwemo baraza, km ktk bajeti yake hakuna hii mipango, ina maana
muziki wetu wa dansi, utahitaji taasisi nyingine kuuinua, kwani kutokuwa na
public social Hall, kuna changia muziki wetu kuendelea kudorola. Nakumbuka sera
za zamani kila kampuni au kiwanda au taasisi ilikuwa na sehemu ya burudani hata
michezo, ndio maana had Leo miziki ya zaman itaendelea kukumbukwa sana kuliko
hii ya sasa, haijalishi umehit mara ngap, utapigwa Radio mara kadhaa basi
wanauchoka, inakuwa km "bublish " watafuna ikiisha utamu tu waitema.
14. mikoani na wilayani kunakua na
hizo nyingi halafu miji mikubwa kunakuwa na viwanja vikubwa vya burudani vya
kisasa vinavyomilikiwa na serikali
15. [09:31, 6/23/2017] Lkn hivi ktk
bunge, cjasikia wabunge wakijadili hata uwepo wa hizi bendi zetu kongwe, mara
nyingi wanaishia " kuselebuka " ,ebu wekeni "jojina " yaan
wanacheza na kuimba tu
[09:33, 6/23/2017] Wana mchango
mkubwa wa kuzirudisha hizi bendi zetu na kuzihuisha tena, zikawa na uhai na
ushindani na bendi nyingine, kuliko kutegemea "Gate collections "
[09:35, 6/23/2017] Tukizungumzia
hizi kumbi, lazima tuzizungumzie bendi zetu
pia, maana watakuja kusema, kumbi za nini wakati muziki wenyewe hauone
kani dah, uwa naumia sn na huu muziki wetu.
16. nadhani tukipata mtu akawa ama
Wazir ama mbunge itasaidia,vinginevyo vyama vya muziki haswa wa dansi,kama
yatakubaliwa basi itakuwa poa,mfano sera ya mheshimiwa Rais ya Tanzania ya
viwanda,wizara nayo ingetumbukiza mkono ikasema viwanda na burudani kuweka
uanzishwaji wa viwanda kwenda sambamba na shughuli za burudani mbalimbali pamwe
na muziki mfano kama ilivyokuwa bima nk,Jumuiya mbalimbali nazo ziamshe
burudani nk
17. [09:43, 6/23/2017 Hii itarudisha kirahisi muziki wetu, twahitaji watu wenye uzalendo ktk
hili
[09:45, 6/23/2017 Mfano mimi binafsi ningekuwa na uwezo ili kuteka "hadhira " kirahisi,
basi ningekusanya wana muziki wote mahiri na ninaojua hawa wapo vzr, ningeingia
nao mkataba wa miaka 3-5 ,na wakitoa album, mbili tatu, dah lazima watu
wakubali
[09:47, 6/23/2017 Yaan ntafanya km vile "Tanzania all stars " ikishindikana hapo basi
tutakuwa tumerogwa.
18. kile kiwanda cha kuunganisha
matrekta kibaha kinakuwa na bendi inaitwa Valment jazz band si mchezo
19. [09:51, 6/23/2017 haiwezi kushindikana,ujue kwa hii kauli mbiu ya viwanda inaenda na kukua kwa
ajira na kuongezeka kwa mzunguko wa pesa ktk eneo husika hivyo si rahisi kukosa
watu,lkn pia lengo la kwanza ni kuburudisha wafanyakazi siku za mapumziko kwa
hiyo hata wale wafanyakazi watakaofanya mtoko weekend wanaanzia kwao,na wake
zao,watoto ndugu jamaa na marafiki hebu ona hapo
[09:54, 6/23/2017 Ngoja kgt ikue, tumiliki bendi ya mfano
20. Hakika utu uzima dawa
21. Hii nzuri. Monkeys and nami
nawaza hizi community centers kwa nini hatuoni umuhimu wake...vijijini pia hali
mbaya. Choice ni kushinda kilabu au kanisani haswa msimu usio na shughuli za
kilimo
22. Nimependa andiko hili. Sahihi
kabisa! Niliwahi kuandika kuhusu uvunjaji wa majengo DSM na kuporomosha sky
scrapers, hatukatai lakini tunaondoa historia ya jiji letu ambapo tungeweza
kujenga new dsm na kuiacha old DSM kama ilivyo kwani historia ambayo
inafundishwa shuleni na picha zilizopo haipo ukija katika uhalisia. Mfano
nilifika mji wa Bulawayo Zimbabwe wanao mji unaitwa old pumula na new
pumula,ambapo wamefanikiwa kuhifadhi historia ya mji wao hawajaubomoa na Leo ni
kivutio tosha cha utalii. Hili nimeliongea Facebook zaidi ya Mara 2. Nashukuru
kwa andiko hili kwani linaakisi mawazo yangu kuhusu uhifadhi. Siku njema!
23. [09:05, 6/23/2017 Kabisa! Matokeo yake tunaanza kupambana na changamoto ya foleni,maeneo ya
maegesho ya magari,mafuriko katikati ya jiji kwa sababu tu ya kutaka
kulazimisha mambo na kuacha uasilia wake! Itaendelea kutugharimu sana
[09:08, 6/23/2017 Kuanzia Zinga,bagamoyo,mlandizi,ruvu,chalinze,kibaha,pugu,kisarawe,chanika na
kwingineko pembezoni,pangeweza kujenga new DSM na kuacha jiji kama lilivyokuwa.
Leo hii barabara nyingi zimebadilishwa,njia uliyopita mwezi jana ukipita leo
unakuta kibao (no entry)! Balaa hili!
[09:13, 6/23/2017 Majengo makubwa yameongezeka tena mengi pale kkoo,lakini miundombinu ipo ileile
ingawa kunakipindi wachina waliongeza miundombinu lakini haijasaidia kitu kuna
mitaa ukipita Maji ya chooni yanamwagika kana kwamba ni kitu cha kawaida,wazo
lakujenga Dar mpya ramani ya kisasa ingekua poa sana
[09:16, 6/23/2017Sugu lifikishe kwa waziri kivuli wa mazingira......
24. Asante Mzee Kitime, umegusa
sehemu nzuri na mhimu kwa vijana wa taifa hili hasa ukizingatia vijana wengi
wamekuwa na mwamko wa sanaa huku wakijiendesha wenyewe bila msaada wowote toka
serikalini, niliwahi kumwambia kitu hiki mwakilishi mmoja toka wizarani
alitutembelea hapa nafasi siku Za nyuma, community center Ni mhimu sana kwa
vijana hata huku walikoendelea bado vipo na vijana wanatumia hadi leo, viongozi
wetu alifanyie kazi siyo vijana wote wapenda soka!!!!!
hizi ni baadhi tu ya mesej zilizotumwa kupitia group za whatasapp. Kuna maoni yanendelea kutolewa kupitia Instagram na hata kupigiwa simu....kuna haja ya kuwaamsha viongozi ili kuwanusuru vijana wa nchi hii kwa balaa zaidi....
Comments