Katika video hii mtangazaji anadai kuwa aliwauliza wanasheria wanaofahamu 'mambo kama haya' akimananisha haki za msanii katika sheria za hakimiliki. Na mtangazaji akadai kuwa aliambiwa kuwa haki inalindwa ikiwa tu kazi ilisajiliwa katika 'Baraza' husika. Hii si kweli. Tanzania ikiwa ni mmoja wa signatories wa Berne Convetion toka mwaka 1994, hulinda kazi zozote za hakimiliki kuanzia pale inapoweza kushikika, na bila kujali ubora wa kazi yenyewe. Hakuna kipengele kinacholazimisha usajili popote kabla ya kuanza kulindwa na sheria, na sheria yetu ya Hakimiliki (Copyright and Neighbouring Rights Act no 7 of 1999) pia inalinda haki za mtunzi kwa msingi huo. Hivyo wasanii/watunzi wasipotoshwe kuwa ni lazima kazi yako iwe imesajiliwa ndipo itakapoanza kulindwa. Kusajili kunakusaidia kupata haki zako nyingine kama vile kukusanyiwa mirabaha, na pia huongeza ushahidi wakati wa kesi za madai kama hizi.
John Kitime
Comments